(ABNA24.com) Lieberman, kiongozi wa chama cha 'Yisrael Beiteinu' ameyasema hayo kupitia ujumbe aliomtumia siku ya Jumapili Benny Gantz, Kiongozi wa Chama cha Blu na Nyeupe ambaye pia kwa sasa ndiye Spika wa Bunge la Utawala wa Kizayuni, Knesset. Katika ujumbe huo Avigdor Lieberman amemtaka Gantz kuandaa mazingira ya kupitishwa mpango wa kumzuia Netanyahu kuhudumu kwenye nafasi hiyo. Waziri huyo wa zamani wa vita wa utawala katili wa Kizayuni amebainisha kwamba, hivi sasa Netanyahu anapoteza muda tu na wala hataki kutia saini mapatano waliyotiliana saini na Benny Gantz mwenyewe.
Hii ni katika hali ambayo maelfu ya raia wa utawala haramu wa Kizayuni Jumapili walifanya maandamano wakilalamikia kucheleweshwa muda wa kuundwa serikali suala linaloendelea kuwadhuru kutokana na kuenea virusi vya Corona. Mazungumzo ya vyama viwili vya Likud na Blu na Nyeupe yamekwama kutokana na pendekezo la Netanyahu la kutaka kupitishwa sheria itakayoizuia mahakama kuu ya utawala huo kumuuzulu katika nafasi yake ya uwaziri mkuu.
.............
340